Matt son sang
Twasikitika moyoni, huenda ikawa aushini,
Serikali jameni, kwani tulichagua nani?
Mhalifu mlangoni, japo hamuoni, Mwalala kitandani, wananchi mashakani,
Ukuta tutaujenga, iwapo ufa hautazibwa.
Wakenya wasio na hatia, kila mara tunawapoteza,
Wazazi na marafiki wanalia, serikali muwape mwangaza,
Ni lipi serikali mwanuia? Wakenya machungu wanameza,
Hadi lini mhalifu atatuingilia? Wakenya moyoni wajiuliza,
Ukuta tutaujenga, iwapo ufa hautazibwa.
Rais na mawaziri, walinzi wamewazingira,
Mwandishi wa hili shairi, wahalifu wamemzingira,
Ni wakati gani mutakiri, kupuuza huleta madhara?
Viongozi sio siri, mwafananishwa na “mutura”
Ukuta tutaujenga, iwapo ufa hautazibwa
Siasa mumeipa kipau mbele, waliowachagua mnawapa kisogo,
Bungeni mwapiga kelele, ahadi zenu zageuka uwongo,
Wakenya machozi tele, tamaa kuu kugeuka udongo,
Wakenya twajuta milele, adui wetu mkuu ni hongo
Ukuta tutaujenga, iwapo Ufa hautazibwa
Comments
Post a Comment