Matt son sang Siku chache baada ya madai kuwa kiongozi wa wadi la saimo/Kipsaraman, alichochea kufungwa kwa naibu wa Rais mheshimiwa William Rutto na kuachiliwa kwa mtangazaji Joshua Sang, waliompigia kura waanzisha shuguli za kumuondoa mamlakani. Bwana Tekelon alijipata motoni baada ya kuinua karatasi lililoandikiwa madai hayo huku akijiunga na walimu Katika maandamano ya kuongezwa kwa mshahara Yao. Wakaazi wa wadi wametangaza kusikitishwa na kitendo hicho na kuwa yalikuwa matamshi yake na siyo ya Wakaazi hao kama ilivyosemwa hapo awali. Kulingana na wakaazi wa wadi hilo, bwana Tekelon aliwahusisha na kitendo kisichowafurahisha ndiposa wananuia kumgoa mamlakani.