Matt son sang
Wanakijiji wa korokorwonin kaunti ya Baringo wapigwa na mshangao baada ya nyumba kuteketea licha ya madai kuwa moto haukuwa umewashwa mle ndani.
Wafanyi biashara waliokuwa Katika pilka pilka zao za kutafuta pesa, walilazimika kufunga biashara zao ili kuzima moto huo. Juhudi zao ziligonga mwamba baada ya nyasi iliyotumika kujenga nyumba hiyo kushika moto. "tulijaribu kuzima lakini hatukuweza kwa sababu ilikua nyumba ya nyasi" alisema kipruto mmojawao wa waliofika mapema kwa minajili ya kuzima moto huo.
Kulingana na wanakijiji wa eneo hilo, ni mara ya pill nyumba kuteketea Katika familia hiyo.
Utafiti ungali bado unafanyika kubaini kiini cha moto huo.
Comments
Post a Comment