Matt son sang
Nilienzi mapenzi nikindhani nimemaliza,
Nikasahau ujinga huepukwa Kwa kuuliza,
Ngoja ngoja huumiza matubo nilidhani mwangaza,
Bila kujua mwishowe ningejutia kutowaza.
Kwei, mapenzi kuenzi ni machozi mtetezi.
Mapenzi muhimu, jukumu lako kujitolea,
Mapenzi ni sumu utumiapo visivyo, hujuta kujikojolea,
Mapenzi ya dhati yape ulinzi, isije ikakupotelea,
Mapenzi kuyapoteza, jeraha moyoni utaulea.
Kweli, mapenzi kuenzi ni machozi mtetezi.
Mapenzi sikizeni, yaongoza duniani,
Tumia kwa umakini, yasikutie mashakani,
Ndwele sikizeni, unazambaa ardhini,
Uamuzi mikononi, akili kichwani,
Kweli, mapenzi kuenzi ni machozi mtetezi.
Mapenzi ni maua, maulana katupea,
Ilhali yaua, unapozembea,
Mapenzi matamu, iwapo utajitolea,
Ilhali machungu, inapolegea.
Kwei, mapenzi kuenzi ni machozi mtetezi
Comments
Post a Comment