Sarah moyoni twasikitika, machozi yatiririka,
Moyoni twajiuliza, nani kakupeleka. Chuoni twakumbuka, moyo nzuri wa kutajika,
Mazuri ukatupa, baraka zako ukatupa.
Sarah uko wapi, nani kakupeleka?
Kila tunapopumzika, mawazo yatiririka,
Sura yako ya kutajika, akilini yachoreka.
Sauti yako yasikika, kila pahali twajipeleka,
Taswira zako zapangika, kila tunapoamka.
Sarah uko wapi, nani kakupeleka?
Bidii yako ya mchwa twakumbuka, hadi tutakapopumzika,
Maanake kupumzika, kila mmoja hutarajia,
Uhai maulana katupa, vile vile uhai kachukua,
Sababu kuu ajua, mmojawapo akupenda.
Sarah uko wapi, nani kakupeleka?
Twatumai kukutana, huko kwake maulana,
Maanake hii dunia, sio nyumbani hakika,
Wakati mwema pahali pema, afya njema maisha mema,
Safiri salama, msalimu maulana.
Sarah uko wapi ' nani kakupeleka??
RIP DIA SARAH WE LOVE YOU
Comments
Post a Comment